Mwanafunzi
mmoja kwa jina Joseph Owino kutoka Musikoma eneobunge la Kanduyi kaunti ya
Bungoma amejiwasilisha katika shule ya wavulana ya Ndivisi akiwa
na barua yake pekee, bila mzazi, na vifaa muhimu vya masomo.
Owino
ambaye ni alipata alama 338 katika shule
ya Moi Primary anasema juhudi zake za kupata msaada kutoka kwa eneobunge la CDF
la Kanduyi ziligonga mwamba na alipoona siku za kuripoti zinaisha aliamua
kutembea kwa miguu kutoka Musikoma hadi Shule ya Wavulana ya Ndivisi eneobunge la Webuye Mashariki.
“mamangu
huchoma Mahindi na nina Ndugu zangu ambao pia wanamtegemea, alijaribu kutafuta
karo lakini njia zote zikashindikana,” Owino alisema.
Owino
ambaye alikuwa tu na barua na sare ya shule ya msingi na patipati zilizochanika
anatoa wito kwa wahisani akiwemo mbunge
wa Kanduyi John Makali na gavana wa kaunti ya Bungoma Keneth Lusaka kumsadida
ili alipe karo na kumuwezesha kutimiza ndoto yake ya kuwa daktari.
“Mbunge Wangu Joh Makali naomba
unihurumie unisaidie hata Basari niendelee na masomo yangu nikuwe Daktar.” Alisema
Aemuomba wakilishi wadi eno hilo Bw Makabichi pia kumsaidia afanikishe donto zake.
Mwalimu
mkuu wa shule ya Wavulana ya Ndivisi Martin Wachiye alimpokea mwanafunzi
huyo lakini anatoa wito kwa wahisani kujitokeza na kumlipia karo ili atimize
ndoto yake.