Mwanahararakati wa sasa kaunti ya Bungoma John Wanyama anataka serikali ya kaunti ya Bungoma kufufua kiwanda cha maziwa cha kimalewa.
Akizungumza akiwa wadi ya Mukuyuni eneo binge la kabuchai kwenye hafla moja ya mazishi Wanyama amelaumu viongozi waliochaguliwa kwa kuwasahau wananchi na kuacha viwanda muhimu kaunti ya Bungo kuanguka kikiwemo cha maziwa cha Kimalewa.
"Hii Bungoma viwanda vyote vimeanguka, hiki cha maziwa pia hakuna kiongozi anakishughulikia, naomba gavana Lusaka na na spika Moses wetangula wasaidie watu wetu," Wanyama alisema.
Ameelezea kusikitishwa kwake na pia kiwanda cha maziwa cha webuye ambacho hakijaanza kufanya kazi licha ya serikali kutumia pesa nyingi kukijenga
Wanyama ambaye ametangaza nia ya kuwania useneta mwaka wa 2027 anataka wakaazi wa kaunti ya Bungoma kumchagua viongozi watakaotetea maslahi yao.
