Monday, 10 June 2024

PALANG'A AONYA WABUNGE DHIDI YA MSWAADA WA FEDHA

Huku waziri wa fedha Njuguna Ndung’u  akitarajiwa kusoma makadirio ya bajeti ya mwaka 2024/2025,Mwakilishi wadi ya Olkaria Peter Palang’a anataka wabunge kuondoa ushuru kwa bidhaa muhimu.



Akizungumza akiwa Bokoli kaunti ya Bungoma  Palan’ga amesema  serikal inawadhulumu wananchi kwa kuongeza ushuru wa bidhaa muhimu licha ya Rais Willia Ruto kuahidi kwamba angewasaidia kupunguza ghrama ya maisha

“Kuna watu wanamdanganya Rais na kumshauri apandishe ushuru wa bidhaa muhimu, tunamuomba akumbuke ahadi alizotoa kwa mwananchi wa kawaida wakati wa kampeni,” Palang’a alisema.

Palang’a ambaye amekuwa mwakilishi wadi wa Olkaria kwa miaka 20 anataka wabunge kuangazia mswada wa fedha wa Mwaka wa 2024/2025  akisema watakuwa na maswali ya kuwajibu wakenya waliowachagua.

“Wabunge wetu tunawasihi muangazie kilio cha wakenya, wanaumia na gharama ya ju ya maisha na kuongeza ushuru mwingine kutaendelea kuwaumiza zaidi,” aliongeza

Palanga alisema haya kwenye hafla ya kufuzu kwa wanafunzi wa masomo ya teknolojia kutoka eneobunge la Webuye Magharibi.

Kwenye mradi huo zaidi ya wanafunzi mia tano wamepokea mafunzo ya  teknolojia yanayofadhiliwa na Peter Palang’a huku akitaka vijana zaidi kujitokeza ili wanufaike na masomo hayo .



BUNGOMA HAINA SENETA MCHAPAKAZI-WANYAMA ADAI

 Mwanaharakati wa siasa John Wanyama anataka wakaazi wa kaunti ya Bungoma kuchagua viongozi walio na uwezo wa kuwawakilisha vyema Bungeni.



Akizungumza katika hafla moja ya mazishi Malaha Webuye Magharibi Wanyama amewasuta Wabunge na maseneta kwa kushindwa kumtetea mwananchi wa kawaida na badala yake kuwakilisha tumbo zao Bungeni.

"Munaona gharama ya maisha inapanda kwa sababu ya wabunge tuliowachagua, wanaruhusu serikali kupandisha bei ya bidhaa muhimu na kumnyanyasa mwananchi", Wanyama alisema.

Wanyama ambaye pia ametangaza azma yake ya kuwania kiti cha useneta kaunti ya Bungoma anasema seneta wa sawa David Wakoli hana makali ya kumtetea mkaazi wabungoma katika bunge la seneti.

Anataka wakaazi kumchagua kwenye uchaguzi mkuu ujao akisema seneta wa sasa ameshindwa kutekeleza wajibu wake.

Ameongza kiwa kaunti ya Bungoma kwa sasa Haina mwangalizi wa serikali jambo ambalo linaruhusu ufisadi kuendelea