Huku waziri wa fedha Njuguna Ndung’u akitarajiwa kusoma makadirio ya bajeti ya mwaka 2024/2025,Mwakilishi wadi ya Olkaria Peter Palang’a anataka wabunge kuondoa ushuru kwa bidhaa muhimu.
“Kuna
watu wanamdanganya Rais na kumshauri apandishe ushuru wa bidhaa muhimu,
tunamuomba akumbuke ahadi alizotoa kwa mwananchi wa kawaida wakati wa kampeni,”
Palang’a alisema.
Palang’a ambaye amekuwa mwakilishi wadi wa Olkaria
kwa miaka 20 anataka wabunge kuangazia mswada wa fedha wa Mwaka wa
2024/2025 akisema watakuwa na maswali ya
kuwajibu wakenya waliowachagua.
“Wabunge wetu tunawasihi muangazie kilio cha
wakenya, wanaumia na gharama ya ju ya maisha na kuongeza ushuru mwingine
kutaendelea kuwaumiza zaidi,” aliongeza
Palanga alisema haya kwenye hafla ya kufuzu
kwa wanafunzi wa masomo ya teknolojia kutoka eneobunge la Webuye Magharibi.
Kwenye mradi huo zaidi ya wanafunzi mia tano wamepokea
mafunzo ya teknolojia yanayofadhiliwa na
Peter Palang’a huku akitaka vijana zaidi kujitokeza ili wanufaike na masomo
hayo .
No comments:
Post a Comment