Kama njia mojawapo ya kuimarisha maisha ya wakaazi wa eneo bunge la Webuye mashariki hasa kinamama, afisi ya ustawishaji eneo bunge hilo NGCDF imetoa mkopo wa zaidi ya shilingi laki saba kwa vikundi sita kutoka wadi ya Mihuu ili kuvisaidia kuanzisha miradi mbalimbali.
Akizungumza baada ya kutoa hundi hizo kwa vikundi hivyo, mbunge wa eneo hilo Martin Pepela Wanyonyi amesema kuwa afisi ya NGCDF eneo hilo ameanzisha zoezi hilo ili kuimarisha maisha ya kinamama na wakaazi wa eneo hilo kwa jumla huku akisema kuwa zoezi hilo litaendelea katika eneo bunge lote la Webuye mashariki huku akivirai vikundi vingine kutuma maombi ya kupata fedha hizo.
"Nikisema nitatembea na nyinyi, huu ndii wakati na ninataka hizi pesa muzitumie vizuri ili mujie deleze," Wanyonyi alisema.
Mbunge huyo hata hivyo amevitaka vikundi vilivyonufaika na mkopo huo kutumia fedha hizo vyema na kurudisha kwa wakati ili vikundi vingine vinufaike, kauli iliyoungwa mkono na naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Webuye mashariki Peter Yegon.
Ameahidi pia kulipia vikundi ambavyo havina vyeti Ili pia visajiliwe.
"Wale ambao hamjassjiliwa muje afisini mwangu nitawalipia ili nao pia wanufaikwe," aliongeza.
Hata hivyo ameonya askari wa kaunti dhidi ya kuhangaisha wafanyibiashara wadogowadogo akisema hataruhusu hukka hiyo kuendelea webuye mashariki
MWISHO

No comments:
Post a Comment