Waathiriwa wa ugonjwa wa Saratani kaunti ya Bungoma wameanzisha miradi ya kuwainua kiuchumi ili kukabiliana na changamoto za kifedha wanazokumbana nazo
Mkurugenzi wa
shirika la Better World Daktari Esther Ndare ambaye pia ni mwathiriwa amesema
wamechukua hatua hii baada ya jamaa zao kuwatenga kutokana na gharama ya juu ya
matibabu,
“wengi wetu hawana pesa za matibabu huku wengine wakiwa wamebakia bila pesa
zozote zabaada ya kupata matibabu, miradi kama ya kuku, kushona na kilimo
itatufaidi,” alisema
Hata hivyo wametoa
wito kwa serikali ya kaunti kuimarisha huduma za matibabu za matibabu ya
saratani ili kupunguza mzigo wa kutafuta matibabu hayo Eldoret.
“Ikiwa serikali itaanza kutoa matibab
![]() |
| KUSHOTO DK ESTHER NDARE NA WAATHIRIWA WA SARATANI |
u ya saratani hapa Bungoma tutapunguza safari za kuenda eldoret kutafuta matibabu.” Bi Ndare alisisitiza.
Waathirwa wa saratani waliopona wanasema wamepitia hali ngumu ya Maisha wakitaka wale ambao hawajajua hali zao kutembelea vituo vya afya na kupimwa.

No comments:
Post a Comment