Monday, 17 July 2023

Wewe Eugine tutakunyorosha ukimbie Kimbikimbi - MCA Grace

 Mwakilishi wadi ya sitikho Grace sundukwa amemuonya kinara wa chama Cha DAPK Eugene Wamalwa kwamba takimbia kama mburukenge ikiwa atajaribu kufanya maandamano kaunti ya Bungoma.

Hon Grace Sundukwa-MCA stikho


Bi sundukwa amemshutumu Wamalwa kwamba ni mnafiki na kwamba alijifaidi kupitia jamii ya Bukusu alipokuwa waziri lakini hakuwakumbuka kamwe.

"Nakwambia Engine ukijaribu kuleta kiherehere chako Bungoma tutakukimbiza kama mburukenge Kimbikimbi,' bi sundukwa alisema.

Amemtaka Eugine kuwaambia wakaazi wa kunti ya Bungoma alichofanya alipokuwa waziri kwa muda wa Miaka kumi.

"Wewe Eugine umekuwa waziri wa ugatuzi, maji na ulinzi na haukusaidia muluhya yeyote kupata kazi, ulikula peke Yako Sasa ndio unakuja kutudanganya na gharama ya maisha, tunakupatia red card, fanyia mandamano huko kwenu kitale hapa tutakuonyesha kilichomtoa kanga manyoya," alisisitiza.

Haya yanajiri baada ya fununu kuenea kwamba  Marengo wa azimia unapanga maandamano webuye na bungoma

No comments:

Post a Comment