Thursday, 6 July 2023

WANAFUNZI WADI YA MATULO WAPOKEA BASARI KUTOKA KWA SONKO

 

Mwakilishi wadi ya Matulo Stephen Kaiser Simiyu amepeanan basari kwa   Wanafunzi  kutoka wadi yake huku ikiwa mara ya kwanza wanafunzi wengi kunufaika na basari ikilinganishwa na miaka ya hapo awali.

Akizungumza baada ya kuzindua zoezi hilo katika shule mbalimbali eneo hilo,mwakilishi wa wadi ya huyo  Stephen Kaiser amesema awamu ya kwanza ya shilingi milioni mbili imetolewa katika shule mbalimbali na kuwataka wazazi ambao hawajapokea fedha kwa sasa kuwa na subira huku hawamu ya pili ikitarajiwa hivi karibuni.



“Niliahidi kwamba nitasaidia wanafunzi wasiojiweza kupata masomo , kwa hivyo wale wazazi ambao hawajapata  tutawapa katika awamu ya pili wasiwe na wasiwasi,” Kaiser alisema.

STEVE KAISER- MCA MATULO


Kaiser hata hivyo amewataka wanafunzi walionufaika na fedha hizo kutia bidii masomoni mwao ili waweze kuafikia malengo yao maishani mwao.

hatutakubali kumalizia pesa za umma kwa mwanafunzi anayefanya vibaya katika masomo yao, musipoweka bidii mutakuwa munaharibi masiha yenu ya mbeleni,” alisistiza

Baadhi ya shule zilizonufaika ni kama vile, Shule ya wasichana ya Matulo, shule ya upili ya malaha, St Mathews na  zingine.

No comments:

Post a Comment