Monday, 17 July 2023

Wewe Eugine tutakunyorosha ukimbie Kimbikimbi - MCA Grace

 Mwakilishi wadi ya sitikho Grace sundukwa amemuonya kinara wa chama Cha DAPK Eugene Wamalwa kwamba takimbia kama mburukenge ikiwa atajaribu kufanya maandamano kaunti ya Bungoma.

Hon Grace Sundukwa-MCA stikho


Bi sundukwa amemshutumu Wamalwa kwamba ni mnafiki na kwamba alijifaidi kupitia jamii ya Bukusu alipokuwa waziri lakini hakuwakumbuka kamwe.

"Nakwambia Engine ukijaribu kuleta kiherehere chako Bungoma tutakukimbiza kama mburukenge Kimbikimbi,' bi sundukwa alisema.

Amemtaka Eugine kuwaambia wakaazi wa kunti ya Bungoma alichofanya alipokuwa waziri kwa muda wa Miaka kumi.

"Wewe Eugine umekuwa waziri wa ugatuzi, maji na ulinzi na haukusaidia muluhya yeyote kupata kazi, ulikula peke Yako Sasa ndio unakuja kutudanganya na gharama ya maisha, tunakupatia red card, fanyia mandamano huko kwenu kitale hapa tutakuonyesha kilichomtoa kanga manyoya," alisisitiza.

Haya yanajiri baada ya fununu kuenea kwamba  Marengo wa azimia unapanga maandamano webuye na bungoma

Friday, 14 July 2023

Dondoo za shule ya ACK webuye

 Huenda shule ya msingi ya Webuye ACK ikadidimia kutokana na  mzozo baina ya Bodi ya shule, walimu na mwalimu mkuu bi Tabitha Okiru.

Webuye ACK Primary


Dukudui zinasema......:

kwamba bodi ya shule hiyo chini ya mwenyekiti wake na mwenyekiti wa PTA walikuwa na mazoea ya kushinda shuleni kuanzia jumatatu Hadi ijuuma  lakini alipoingia mwalimu mkuu  mpya  hulka hiyo ilisitishwa jambo ambalo halikuwafurahisha na kuibua vita baridi.

Inadaiwa kwamba huenda mifereji ya kufuja pesa ilizibwa ikibainika kuwa mwalimu mkuu aliyestaafu hakuwa na nafasi ya kusimamia vyema shule hiyo kutokana na udhaifu wa kiafya. 

Hatua hii iliipa bodi ya shule  nafasi ya kutawala shule hiyo.

Dondoo ya pili inasema kwamba  mmoja wa watawala wa kaunti kijijini(village admin) ana ushawishi mkubwa. Inasemekana kwamba amedinda kujiuzulu kama mwalimu licha ya kuajiriwa na kaunti ya Bungoma. Inasemekana kwamba  anatumia nafasi yake serikalini kuvuruga uongozi wa shule huku wanasiasa Fulani webuye mashariki pia wakihusika.

Dondoo ya tatu inasema kwamba Kuna kiongozi mkuu wa chama cha walimu Kaunti ya bungoma  anayetaka jamaa wake wa karibi achukue nafasi ya mwalimu mkuu   na kuwepo kwa bi Okiru ni kizingiti. Anatumia mzozo uliyopo kuvuruga zaidi  ili jamaa wake apate nafasi ya ya kuongoza shule hiyo inayoaminika kuw na donge nono.

Dondoo ya nne insema kuwa matamshi ya bi Okiru kwamba shule hiyo itafanya vyema  bila matokeo ya GMO iliwakera walimu na kuibua vita baridi kutoka kwa walimu.

Dondoo ya Tano inasema kuwa afisi ya elimu bungoma imeshindwa kutegua kitendawili cha mzozo katika shule ya ACK.

Ikiwa kamati ya shule haitadhibitiwa  na uhusiano wa mwalimu mkuu na walimu pia kuchunguzwa huenda shule hiyo ambayo imekuwa ikifanya vyema ikadidimia.

Msukumo kutoka nje pia unafaa kudhibitiwa na viongozi wa kisiasa pia wajiepushe na shule hiyo. 

Dondoo ya sita inasema  kuwa njama ya kupanga maandamano  mara tatu kumtimuwa mwalimu mkuu iligonga mwamba baada ya watu waliokuwa wamelipwa kufanya hivyo kudinda kutumika kufanya hivyo. Maamdamano yanayodaiwa kupangwa na watu Fulani yaligonga mwamba. 

Mwalimu mkuu wa shule hiyo aliletwa baada ya kuidhinishwa na askofu wa kanisa la kianglikana na mbunge wa webuye mashariki ikitarajiwa kwamba ataimarisha matokeo ya shule hiyo zaidi. 


Thursday, 6 July 2023

WANAFUNZI WADI YA MATULO WAPOKEA BASARI KUTOKA KWA SONKO

 

Mwakilishi wadi ya Matulo Stephen Kaiser Simiyu amepeanan basari kwa   Wanafunzi  kutoka wadi yake huku ikiwa mara ya kwanza wanafunzi wengi kunufaika na basari ikilinganishwa na miaka ya hapo awali.

Akizungumza baada ya kuzindua zoezi hilo katika shule mbalimbali eneo hilo,mwakilishi wa wadi ya huyo  Stephen Kaiser amesema awamu ya kwanza ya shilingi milioni mbili imetolewa katika shule mbalimbali na kuwataka wazazi ambao hawajapokea fedha kwa sasa kuwa na subira huku hawamu ya pili ikitarajiwa hivi karibuni.



“Niliahidi kwamba nitasaidia wanafunzi wasiojiweza kupata masomo , kwa hivyo wale wazazi ambao hawajapata  tutawapa katika awamu ya pili wasiwe na wasiwasi,” Kaiser alisema.

STEVE KAISER- MCA MATULO


Kaiser hata hivyo amewataka wanafunzi walionufaika na fedha hizo kutia bidii masomoni mwao ili waweze kuafikia malengo yao maishani mwao.

hatutakubali kumalizia pesa za umma kwa mwanafunzi anayefanya vibaya katika masomo yao, musipoweka bidii mutakuwa munaharibi masiha yenu ya mbeleni,” alisistiza

Baadhi ya shule zilizonufaika ni kama vile, Shule ya wasichana ya Matulo, shule ya upili ya malaha, St Mathews na  zingine.

SARATANI SIO MWISHO WA MAFANIKIO- DKT. ESTHER NDARE

 Waathiriwa wa ugonjwa wa Saratani kaunti ya Bungoma wameanzisha miradi ya kuwainua kiuchumi ili kukabiliana na changamoto za kifedha wanazokumbana nazo

Mkurugenzi wa shirika la Better World Daktari Esther Ndare ambaye pia ni mwathiriwa amesema wamechukua hatua hii baada ya jamaa zao kuwatenga kutokana na gharama ya juu ya matibabu,
wengi wetu hawana pesa za matibabu  huku wengine wakiwa wamebakia bila pesa zozote zabaada ya kupata matibabu, miradi kama ya kuku, kushona na kilimo itatufaidi,” alisema
Hata hivyo wametoa wito kwa serikali ya kaunti kuimarisha huduma za matibabu za matibabu ya saratani ili kupunguza mzigo wa kutafuta matibabu hayo Eldoret.
“Ikiwa serikali itaanza kutoa matibab

KUSHOTO DK ESTHER NDARE NA WAATHIRIWA WA SARATANI

u ya saratani hapa Bungoma tutapunguza  safari za kuenda eldoret kutafuta matibabu.” Bi Ndare alisisitiza.

Anasema shirika la  Better World hupenan pesa za chakula na mahali pa kulala kwa wathiriwa huku akitaka wahisani zaidi kujitokeza na kuwasaidia.
Waathirwa wa saratani waliopona wanasema wamepitia hali ngumu ya Maisha wakitaka wale ambao hawajajua hali zao kutembelea vituo vya afya na kupimwa.