Huenda shule ya msingi ya Webuye ACK ikadidimia kutokana na mzozo baina ya Bodi ya shule, walimu na mwalimu mkuu bi Tabitha Okiru.
 |
| Webuye ACK Primary |
Dukudui zinasema......:
kwamba bodi ya shule hiyo chini ya mwenyekiti wake na mwenyekiti wa PTA walikuwa na mazoea ya kushinda shuleni kuanzia jumatatu Hadi ijuuma lakini alipoingia mwalimu mkuu mpya hulka hiyo ilisitishwa jambo ambalo halikuwafurahisha na kuibua vita baridi.
Inadaiwa kwamba huenda mifereji ya kufuja pesa ilizibwa ikibainika kuwa mwalimu mkuu aliyestaafu hakuwa na nafasi ya kusimamia vyema shule hiyo kutokana na udhaifu wa kiafya.
Hatua hii iliipa bodi ya shule nafasi ya kutawala shule hiyo.
Dondoo ya pili inasema kwamba mmoja wa watawala wa kaunti kijijini(village admin) ana ushawishi mkubwa. Inasemekana kwamba amedinda kujiuzulu kama mwalimu licha ya kuajiriwa na kaunti ya Bungoma. Inasemekana kwamba anatumia nafasi yake serikalini kuvuruga uongozi wa shule huku wanasiasa Fulani webuye mashariki pia wakihusika.
Dondoo ya tatu inasema kwamba Kuna kiongozi mkuu wa chama cha walimu Kaunti ya bungoma anayetaka jamaa wake wa karibi achukue nafasi ya mwalimu mkuu na kuwepo kwa bi Okiru ni kizingiti. Anatumia mzozo uliyopo kuvuruga zaidi ili jamaa wake apate nafasi ya ya kuongoza shule hiyo inayoaminika kuw na donge nono.
Dondoo ya nne insema kuwa matamshi ya bi Okiru kwamba shule hiyo itafanya vyema bila matokeo ya GMO iliwakera walimu na kuibua vita baridi kutoka kwa walimu.
Dondoo ya Tano inasema kuwa afisi ya elimu bungoma imeshindwa kutegua kitendawili cha mzozo katika shule ya ACK.
Ikiwa kamati ya shule haitadhibitiwa na uhusiano wa mwalimu mkuu na walimu pia kuchunguzwa huenda shule hiyo ambayo imekuwa ikifanya vyema ikadidimia.
Msukumo kutoka nje pia unafaa kudhibitiwa na viongozi wa kisiasa pia wajiepushe na shule hiyo.
Dondoo ya sita inasema kuwa njama ya kupanga maandamano mara tatu kumtimuwa mwalimu mkuu iligonga mwamba baada ya watu waliokuwa wamelipwa kufanya hivyo kudinda kutumika kufanya hivyo. Maamdamano yanayodaiwa kupangwa na watu Fulani yaligonga mwamba.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo aliletwa baada ya kuidhinishwa na askofu wa kanisa la kianglikana na mbunge wa webuye mashariki ikitarajiwa kwamba ataimarisha matokeo ya shule hiyo zaidi.