Friday, 10 May 2024

WAT 2 WAAGA BAADA YA KUOKOLEWA KUTOKA JENGO LA KANDUYI


Serikali ya kaunti ungoma imedhibitisha kwamba watu wawili wameaga dunia kufuatia mkasa wa jengo ambalo liliporomoka walipokuwa wakijaribu kuokota vyuma kuuu eneo la kanduyi.

Kwenye ujumbe wake kwa vyombo vya habari gavana wa kaunt ya Bungoma Keneth Lusaka anasema  wiwili hao waliokolewa na maafisa wa mikasa kaunti ya Bungoma na waliaga walipokuwa wakipokea matibabu.

Ripoti kutoka hospitalini inaashiria kwamba wawili hao waliaga baada ya kupoteza damu nyingi.

Gavana Lusaka ameagiza uchunguzi kufanywa na kubaini kwanini jengo hilo halikuangushwa jinsi ilivyokuwa imeratibiwa.

Ameongeza kuwa serikali ya kaunti itawajibikia mazishi ya wawili hao.

 

VUGUVUGU LA MAZINGIRA CONSERVATION LAPANDA MICHE YA MITI 3000 WEBUYE

Kikundi cha kulinda mazingira cha “Mazingira Conservation” kiomeongoza zoezi la upanzi wa miti eneo bunge la Webuye magharibi huku wakipanda zaidi ya miche elfu tatu katika shule eneo hilo.



Mwenyekiti wake Edward Kimakwa anasme kuwa wamekuwa wakiendeleza zoezi la upanzi wa miti katika shule na makanisa eneo hilo na agizo la raisi la kupanda miti linawiana na ajenda ya vuguvugu hilo.

Kimakwa amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Bungoma kupanda miti kwa wingi akiwataka kupunguza ukataji wa miti kiholela.

“Tumekata miti  kwa wingi na huenda kizazi kijacho kikaathirika, kwa sasa hata kuna aina fulani za wanyama na ndege ambao wameadimika kutokana na uharibifu wa mazingira,” Kimakwa alisema

Mwanamazingira huyo ametoa wito kwa viongozi waliochaguliwa kutenga pesa na kununua miche ambayo inaweza kupeanwa kwa wakulima bure ili wapanda.

Ametaka pia serikali ya kitaifa kutobagua waathiriwa wa mvua kaunti ya Bungoma wakati wa kupeana msaada.

“Tuna wakaazi wengi kaunti yetu ya Bungoma walioathirika na mvua inayoendelea, baadhi yao nyumba zimeanguka na wengine mimea yao imeharibiwa na mafuriko, naomba  rais William Ruto  ahakikisha watu wetu pia wanafidiwa kwa hasara waliopata,” Kimakwa alisisitiza.

Kauli yake imeungwa mkono na chifu wa kata ya Miendo Carolye Lwiki  na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya miendo Christine makamu waliowataka wakaazi wa eneo hilo kutumia mvua inayonyesha kwa sasa kupanda miti kwa wingi.

Nao baadhi ya vijana wa kikundi hicho wakiongozwa na katibu wao Nickson Machani wamewataka vijana wenzao kukumbatia upanzi wa miti wakisema huenda ikawanufaisha siku za usoni.

“Vijana wengi hukata tu miti lakini hawakumbuki kupanda, ndio sababu kupitia kwa mfadhili wetu Edward Kimakwa tunapanda miti ili kulinda kizazi kijacho,” Machani alisema


Haya yanajiri wakati ambao taifa la Kenya linashuhudia mvua nyingi huku mamia ya watu wakiathirika  na wengine kuaga dunia.

 

WAHOFIWA KUAGA BAADA YA KUANGUKIWA NA JENGO KANDUYI

Vijana waliokuwa wakiokota vyuma kuukuu kwenye jengo la Wangamati wamefunikwa na vifusi ikihofiwa kwamba huenda wameaga dunia baada ya jengo hilo kuporomoka.

Miongoni mwao ni vijana wanaorandaranda mitaani waliokuwa wakiokota vyuma kutoka eneo hilo.

serikali ya kaunti ya  Bungoma ilianza ubomozi wa jengo hilo linalomilikiwa na familia ya aliyekuwa gavana wa kaunti ya Bungoma Wycliffe Wangamati.

Aliyekuwa gavana Wycliffe wangamati ameisuta serikali ya kaunti kwa utepetevu wake   ambao umepelekea maafa hayo.

kwenye mtandao wake wa kijamii wangamati na Nduguye Winston Wangamati 
wametaka serikali ya kaunti kuwajibikia maafa hayo.


shughuli za uokozi zinaendelea  huku kitengo cha kukabiliana na mikasa kaunti ya Bungoma kikiwa katika njia panda kwa kukosa vifaa vya kukabiliana na mikasa

Thursday, 9 May 2024

AFUENI YA MAJI SAFI MLIMA ELGON

Wakaazi zaidi ya elfu mia moja kutoka mlima elgon, kabuchai na kanduyi  watanufaika na maji safi  baada ya serikali ya kaunti ya Bungoma kwa ushirikiano na  serikai ya Korea kuzindua mradi wa maji eneo la  mlima elgon.



Mradi huo wa maji uliozinduliwa na balozi wa taifa la Korea Yeo Sung-Jun  na gavana wa kaunti ya Bungoma Keneth Lusaka  unalenga kuongeza idadi ya wakaazi wanaopata maji safi ya matumizi.

“Huu mradi wa KOICAII utafaidi wakaazi wetu hapa Mlima Elgon na maeneo bunge jirani kama Kabuchai na kandui na tunalenga kuzindua miradi zaidi ya maji.” Gavana Lusaka alisema.

Balozi wa taifa la Korea amesema mradi huo umegharimu shilingi mlioni mia sita na hivi karibuni  taifa hilo litashirikiana na serikali ya kaunti ya Bungoma kuanzisha mraidi wa KOICA III .



Swala la maji limekuwa donda sugu kwa wakaazi wa kaunti ya bungoma licha ya kuwa na vyanzo vingi vya maji.

Tuesday, 7 May 2024

KITENDAWILI CHA WANGAMATI’S

Familia ya aliyekuwa gavana wa kaunti ya Bungoma Wycliffe wangamati inakadiria hasara baada      ya jumba 

la dhamani ya mamilioni ya pesa kubomolewa kufuatia ujenzi wa uwanja wa Masinde Muliro unaoendelea.

Ujenzi huo unalenga kukamilika kabla ya sherehe za madararka huku serikali ya kaunti ya Bungoma ikibomoa majengo yanayokaribia uwanja wa masinde Muliro.


Familia ya Wangamati Ikiongozwa na aliyekuwa gavana Wyclife Wangamati imekashifu  hatua hiyo ikisema ilipata ardhi hiyo kisheria.

Patrick wangamati ambaye ni mmiliki wa jengoi hilo anasema kuwa alifuata sheria mwaka wa 1968 kupata ardhi hiyo kwa ajili ya Biashara.

“Mimi sio mwizi wa Mashamba, nilifuata sheria na serikali ikanipa ardhi hii na nimekuwa nikiendeleza bisharazangu mahali hapa, nashangaa kwanini wanabomoa nyumba yangu,” Mzee wangamati alisema.

Ubomozi huo umeibua hisia mseto kutoka kwa wafuasi wa aliyekuwa gavana Wycliffe  Wangamati wakimtuhumu gavana Keneth Lusaka na spika Moses Wetangula kwa kumulenga  kisiasa.

Hata hivyo mradi wa ujenzi wa uwanja wa Masinde Muliro ulianzishwa na aliyekuwa gavana Wycliffe Wangamata alipokuwa uongozini. Wakati uo huo alianzisha ujenzi wa barabara kuu mjini Bungoma maarufu kama (dual carriage).

Wangamati alinukuliwa akisema kuwa wale wote waliojenga kwenye ardhi ya serikali waondoe majenge  hayo ili kuruhusu ujenzi wa miradi hiyo miwili mikuu la sivyo serikali itekeleze ubomozi huo.

Wapinzani wake wanadai kuwa alinuia kutumia wadhifa wake kujilinda dhidi ya ubomozi huo.