Friday, 10 May 2024

VUGUVUGU LA MAZINGIRA CONSERVATION LAPANDA MICHE YA MITI 3000 WEBUYE

Kikundi cha kulinda mazingira cha “Mazingira Conservation” kiomeongoza zoezi la upanzi wa miti eneo bunge la Webuye magharibi huku wakipanda zaidi ya miche elfu tatu katika shule eneo hilo.



Mwenyekiti wake Edward Kimakwa anasme kuwa wamekuwa wakiendeleza zoezi la upanzi wa miti katika shule na makanisa eneo hilo na agizo la raisi la kupanda miti linawiana na ajenda ya vuguvugu hilo.

Kimakwa amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Bungoma kupanda miti kwa wingi akiwataka kupunguza ukataji wa miti kiholela.

“Tumekata miti  kwa wingi na huenda kizazi kijacho kikaathirika, kwa sasa hata kuna aina fulani za wanyama na ndege ambao wameadimika kutokana na uharibifu wa mazingira,” Kimakwa alisema

Mwanamazingira huyo ametoa wito kwa viongozi waliochaguliwa kutenga pesa na kununua miche ambayo inaweza kupeanwa kwa wakulima bure ili wapanda.

Ametaka pia serikali ya kitaifa kutobagua waathiriwa wa mvua kaunti ya Bungoma wakati wa kupeana msaada.

“Tuna wakaazi wengi kaunti yetu ya Bungoma walioathirika na mvua inayoendelea, baadhi yao nyumba zimeanguka na wengine mimea yao imeharibiwa na mafuriko, naomba  rais William Ruto  ahakikisha watu wetu pia wanafidiwa kwa hasara waliopata,” Kimakwa alisisitiza.

Kauli yake imeungwa mkono na chifu wa kata ya Miendo Carolye Lwiki  na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya miendo Christine makamu waliowataka wakaazi wa eneo hilo kutumia mvua inayonyesha kwa sasa kupanda miti kwa wingi.

Nao baadhi ya vijana wa kikundi hicho wakiongozwa na katibu wao Nickson Machani wamewataka vijana wenzao kukumbatia upanzi wa miti wakisema huenda ikawanufaisha siku za usoni.

“Vijana wengi hukata tu miti lakini hawakumbuki kupanda, ndio sababu kupitia kwa mfadhili wetu Edward Kimakwa tunapanda miti ili kulinda kizazi kijacho,” Machani alisema


Haya yanajiri wakati ambao taifa la Kenya linashuhudia mvua nyingi huku mamia ya watu wakiathirika  na wengine kuaga dunia.

 

No comments:

Post a Comment