Familia ya aliyekuwa gavana wa kaunti ya Bungoma Wycliffe wangamati inakadiria hasara baada ya jumba
la dhamani ya mamilioni ya pesa kubomolewa kufuatia ujenzi wa uwanja wa Masinde Muliro unaoendelea.Ujenzi huo unalenga kukamilika kabla ya sherehe za madararka
huku serikali ya kaunti ya Bungoma ikibomoa majengo yanayokaribia uwanja wa
masinde Muliro.
Familia ya Wangamati Ikiongozwa na aliyekuwa gavana Wyclife Wangamati imekashifu hatua hiyo ikisema ilipata ardhi hiyo kisheria.
Patrick wangamati ambaye ni mmiliki wa jengoi hilo anasema
kuwa alifuata sheria mwaka wa 1968 kupata ardhi hiyo kwa ajili ya Biashara.
“Mimi sio mwizi wa Mashamba, nilifuata sheria na serikali
ikanipa ardhi hii na nimekuwa nikiendeleza bisharazangu mahali hapa, nashangaa kwanini
wanabomoa nyumba yangu,” Mzee wangamati alisema.
Ubomozi huo umeibua hisia mseto kutoka kwa wafuasi wa
aliyekuwa gavana Wycliffe Wangamati
wakimtuhumu gavana Keneth Lusaka na spika Moses Wetangula kwa kumulenga kisiasa.
Hata hivyo mradi wa ujenzi wa uwanja wa Masinde Muliro
ulianzishwa na aliyekuwa gavana Wycliffe Wangamata alipokuwa uongozini. Wakati uo
huo alianzisha ujenzi wa barabara kuu mjini Bungoma maarufu kama (dual carriage).
Wangamati alinukuliwa akisema kuwa wale wote waliojenga
kwenye ardhi ya serikali waondoe majenge
hayo ili kuruhusu ujenzi wa miradi hiyo miwili mikuu la sivyo serikali
itekeleze ubomozi huo.
Wapinzani wake wanadai kuwa alinuia kutumia wadhifa wake
kujilinda dhidi ya ubomozi huo.
No comments:
Post a Comment