Thursday, 9 May 2024

AFUENI YA MAJI SAFI MLIMA ELGON

Wakaazi zaidi ya elfu mia moja kutoka mlima elgon, kabuchai na kanduyi  watanufaika na maji safi  baada ya serikali ya kaunti ya Bungoma kwa ushirikiano na  serikai ya Korea kuzindua mradi wa maji eneo la  mlima elgon.



Mradi huo wa maji uliozinduliwa na balozi wa taifa la Korea Yeo Sung-Jun  na gavana wa kaunti ya Bungoma Keneth Lusaka  unalenga kuongeza idadi ya wakaazi wanaopata maji safi ya matumizi.

“Huu mradi wa KOICAII utafaidi wakaazi wetu hapa Mlima Elgon na maeneo bunge jirani kama Kabuchai na kandui na tunalenga kuzindua miradi zaidi ya maji.” Gavana Lusaka alisema.

Balozi wa taifa la Korea amesema mradi huo umegharimu shilingi mlioni mia sita na hivi karibuni  taifa hilo litashirikiana na serikali ya kaunti ya Bungoma kuanzisha mraidi wa KOICA III .



Swala la maji limekuwa donda sugu kwa wakaazi wa kaunti ya bungoma licha ya kuwa na vyanzo vingi vya maji.

No comments:

Post a Comment