Kikundi cha kulinda
mazingira cha “Mazingira Conservation” kiomeongoza zoezi la upanzi wa miti eneo
bunge la Webuye magharibi huku wakipanda zaidi ya miche elfu tatu katika shule
eneo hilo.
Mwenyekiti wake Edward
Kimakwa anasme kuwa wamekuwa wakiendeleza zoezi la upanzi wa miti katika shule
na makanisa eneo hilo na agizo la raisi la kupanda miti linawiana na ajenda ya
vuguvugu hilo.
Kimakwa amewahimiza
wakaazi wa kaunti ya Bungoma kupanda miti kwa wingi akiwataka kupunguza ukataji
wa miti kiholela.
“Tumekata miti kwa wingi na huenda kizazi kijacho
kikaathirika, kwa sasa hata kuna aina fulani za wanyama na ndege ambao
wameadimika kutokana na uharibifu wa mazingira,” Kimakwa alisema
Mwanamazingira huyo
ametoa wito kwa viongozi waliochaguliwa kutenga pesa na kununua miche ambayo
inaweza kupeanwa kwa wakulima bure ili wapanda.
Ametaka pia serikali
ya kitaifa kutobagua waathiriwa wa mvua kaunti ya Bungoma wakati wa kupeana msaada.
“Tuna wakaazi wengi
kaunti yetu ya Bungoma walioathirika na mvua inayoendelea, baadhi yao nyumba
zimeanguka na wengine mimea yao imeharibiwa na mafuriko, naomba rais William Ruto ahakikisha watu wetu pia wanafidiwa kwa hasara
waliopata,” Kimakwa alisisitiza.
Kauli yake imeungwa
mkono na chifu wa kata ya Miendo Carolye Lwiki na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya miendo
Christine makamu waliowataka wakaazi wa eneo hilo kutumia mvua inayonyesha kwa
sasa kupanda miti kwa wingi.
Nao baadhi ya vijana
wa kikundi hicho wakiongozwa na katibu wao Nickson Machani wamewataka vijana
wenzao kukumbatia upanzi wa miti wakisema huenda ikawanufaisha siku za usoni.
“Vijana wengi hukata tu miti lakini hawakumbuki kupanda, ndio sababu kupitia
kwa mfadhili wetu Edward Kimakwa tunapanda miti ili kulinda kizazi kijacho,”
Machani alisema
Haya yanajiri wakati ambao taifa
la Kenya linashuhudia mvua nyingi huku mamia ya watu wakiathirika na wengine kuaga dunia.