Maafisa wa polisi mjiini Webuye wanamsaka mwanamke mmoja anayedaiwa kumuachia mwanamke mwingine mtoto wa miezi miwili katika kituo cha kibiashara cha Dina kabla yake kutoweka.
Kulingana na Mary Wanjala aliyeachiwa mtoto huyo anadai kuwa mwanamke huyo alishuka kwenye gari moja akiwa na mizigo kabla ya kumuomba amsaidie kumbebea mtoto huyo ili akavukishe mizigo upande wa pili kabla yake kutoweka kwa kupanda gari la kuelekea mjini Kitale.
Kisa hicho kimekashifiwa na
wakaazi wa eneo hilo huku wakitaka vitengo vya usalama kuanzisha msako dhidi ya mwanamke huyo.
Hata hivyo wakaazi hao wamesema kuwa wataishi na mtoto huyo iwapo wazazi wake hawatapatikana.
MWISHO

No comments:
Post a Comment