Saturday, 13 November 2021

MARTIN WANYONYI(INVESTOR)-NI MIMI PEKE YANGU NAWEZA KUMRIDHI SAMBU-

 

Mwakilishi wadi ya Ndivisi Martin Wanyonyi amesema kuwa yuko katika nafasi bora kumridhi Mbunge wa sasa wa Webuye Mashariki Alfred Sambu.

MARTIN WANYONYI (KATIKATI) AKIWA MAKUSELWA


Akizungumza  akiwa Makuselwa katika Hafla moja ya Mazishi Wanyonyi amesema  ataleta mageuzi makubwa eneobunge la Webuye Mashariki akiwataka wakaazi eneo hilo kumchagua katika uchaguzi mkuu ujao.

“kati ya hawa wanasiasa munaona wakitembea ni mimi pekee yangu niko na rekodi nzuri ya utendakazi, wengine wao wamejihusisha na ukora na ulaghai, sasa wanataka kutuletea ufisadi hapa Webuye East, wakija muwapuuzilie mbali,” wanyonyi alisema.

Wanyonyi ameongeza kuwa akiwa mbunge atahakikisha swala la kupeana basari, kandarasi na ajira litafanywa kwa usawa bila ufisadi.

“Mmejionea vile nimenyorosha wadi ya Ndivisi kwa miaka mitano pekee, mukinipa ubunge hamtajuta kunipa nafasi hiyo,” aliongeza.

 Ameongeza kuwa atapigania haki za wakaazi  likiwemo swala la mlima chetambe chetambe ili wakaaazi wasifurushe katika mashamba yao.

Upinzanimkali unatarajiwa katika uchaguzi mkuu ujao kiti cha webuye mashariki kikivutia wanasiasa wengi akiwemo Caro Buyela na Dkt Iyaya wanjala

No comments:

Post a Comment