Viongozi wa kidini kaunti ya Bungoma wanamtaka kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kujitokeza na kuelimisha wakaazi wa Nyanza kuhusiana na umuhimu wa uwiano na utangamano msimu huu wa siasa.
Hii inakuja Siku chache
tu baada ya msafara wa naibu rais
William Ruto kushambuliwa kwa mawe na baadhi ya vijana katika eneo la
Kondele kaunti ya Kisumu.
Maaskofu hao David
Walukhu na Hamphry Wanyama wamejitokeza
na kukashifu vurugu hizo na kutaka viongozi wa kisiasa kukoma kuwatumia vijana
vibaya wakisema kitendo hicho huenda kikarejesha taifa hili kwenye michafuko ya
kisiasa.
“Itakuwa vyema ikiwa kinara
wa ODM atajitokeza wazi na kujitenga na vurugu hizo na pia ashauri wakaazi wa Kisumu
kudumisha amani jinsi tulivyo ona wakenya wengine walivyofanya katika mikutn
tofauti ya kisiasa inayofanywa na wanasiasa nchini,” akofu Wanyama alisema.
![]() |
| BISHOP HAMPHRY WANYAMA-JESUS TO ALL NATIONS CHURCH |
Askofu walukhu naye
ametaka wanasiasa pia kuhubiri amani kabla ya uchaguzi mkuu ujao akisema mungu
mwenyewe atachagua mtu atakayemridhi rais Uhuru Kenyatta.
“Hatutaki vurugu za
mwaka wa 2007 zirejelewe tena, tunawaomba wanasiasa hasa walewanaowania uraise
wahubiri amanai, hatutaruhusu mwenendo kama uliokuwa Kondele kuendelea nchini wakti
ambapo makovu ya vurugu za mwaka wa 2007 hayajapona,” Akofu walukhu alisema.
![]() |
| BISHOP DAVID WALUKHU-MWENYEKITI WA WAHUBIRI WEBUYE WEST SUBCOUNTY |
Viongozi hao hata
hivyo wamewahimiza vijana kukoma kutumiwa vibaya na wanasiasa hao na badala
yake kujihusisha na maswala muhimu ya taifa.


No comments:
Post a Comment