Wednesday, 10 November 2021

RUDISHENI MICHEZO NA LIKIZO SHULE ZISICHOMEKE- MAASKOFI WAOMBA SEEIKALI

Viongozi wa kidini katika kaunti ya Bungoma wamejitokeza wazi na kukashifu hatua ya wanafunzi wa shule za upili kuteketeza mabweni yao huku wakipendekeza adhabu ya kiboko kurejeshwa shuleni huku pia wakiwalaumu wazazi kwa kuwatelekeza wanao wakiwa nyumbani.

Wakizungumza na wanahabri mjini Webuye,viongozi hao wa kidini wakiongozwa na mwenyekiti wa ushirika wa Webuye Alex Masika na askofu wa kanisa la City harvest Emmanuel Wakhungila wamesema kuwa serikali inafaa kurejesha adhabu ya kiboko shuleni ili kuwaadhibu wanafunzi watundu na kuwataka wazazi kuwajibika katika malezi ya wanao kwa kuwapa muelekeo mwema.


"Watoto siku hizi wanatelekezwa sana, tunaomba adhabu ya viboko irejeshwe shuleni ili kurejesha nidhamu," Askofu Wakhungila alisema.


Viongozi hao wa kidini hata hivyo wanaitaka tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC kusitisha uhamisho wa walimu wakuu wakidai kuwa huenda pia ndicho chanzo Cha visa vya moto shuleni na kutaka pia wizara ya elimu kurejesha michezo shuleni.

"Tumegundua kuwa kuhamisha walimu kiholela kunapelekea kuwepo na upinzani kutoka kwa jamii, walimu, wafanyikazi na wanafunzi wa shule wanakoenda walimu wakuu, kwa hivyo tunaomba TSC isitishe uhamisho wa walimu wakuu kiholela," Askofu Masika alikariri.


Askofu Alex Masika  na Emmanuel wakhungila

 Viongozi hao wa makanisa pia wanataka wizara ya elimu irudishe michezo shuleni wakiwataka walimu pia kuwapa wanafunzi muda wa kupumzika.
"Baada ya korona walimu wanafunza wanafunzi mfulilizo bila mapumziko, hili pia linaweka presha kwa watoto," Wakhungila alisisitiza.

 

No comments:

Post a Comment