Wednesday, 3 November 2021

NAWEZA FANYA KAZI NA WANGAMATI TENA- MOSES WETANGULA



Kinara wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na viongozi wote akiWemo gavana wa kaunti  ya Bungoma Wyclife Wangamati.
 Kulingana na Wetangula ikiwa kutakuwa na maelewano wanaweza kufany kazi tena.
"Hii siasa haina adui wa milele kunaweza kuwa na Handshake na tukaendelea pamoja tena" wetangula alisema
akizungumza akiwa katika stesheni moja ya radio Wetangula anasema kuwa siasa haina chuki na kunaweza kuwepo na uwiano iwapo watu wawili wamekosana.
Wetangula amesema haya licha yake kutangaza kuwa tamuunga Spika wa seneti Keneth Lusaka katika azma yake ya kuwa gavana wa kaunti ya Bungoma tena.

No comments:

Post a Comment