Wajane 150 wamenufaika na msaada wa shilingi 40,000/= kutoka kwa mwaniaji wa kiti cha mwakilishi wadi ya Matulo Steve Simiyu ili kufanikisha miradi katika kikundi Chao.
![]() |
| MWAKILISHI WA WAKFU WA STEV KAISER AKIZUNGUMZA NA WAJANE |
"Kwa muda tumekosa mtetezi wa wajane Matulo, na huu ndio wakati nawaomba mnipe nafasi ya kuwakilisha ili mufurahie uongozi Bora", Simiyu alisisitiza.
Kikundi Cha Balekhwa self help group ni mojawapo ya vikundi vya wajane wadi ya Matulo vilivyonufaika na msaada wa wakfu wa Steven Kaiser.
Msaada wa mabati kwa kanisa Matulo
Kando na wajane kanisa la Hope of God Matulo pia limepokea Mabati 40 kutoko kwa wakfu wa Stev Kaiser ili kukamilisha ujenzinwake.
Kiongozi wa kanisa Hilo Daniel Amunaba anasema imechukua muda mrefu kukamilisha kanisa Hilo akisema msaada kutoka kwa wakfu huo ulio chini ya Steve kaiser Simiyu utawasaidia kukamilisha jengo Hilo.
Muhubiri huyo ameongeza kuwa juhudi zao za kupata ufadhili ziligonga mwamba Hadi walipomfikia Steve sonko.
![]() |
| MAPEMA KABLA KUPELEKA MABATI KANISANI |
Akizungumza na mwandishi wa Makala haya Steve Songo amesema analenga kutoa ufadhili wake kwa makanisa, makundi ya vijana, akina mama na Watu binafsi ili kuinua hali ya maisha ya wakaazi wa Matulo.


No comments:
Post a Comment