Saturday, 19 October 2024

Wanyama ataka kiwanda cha Maziwa kimalewa Kufufuliwa


 Mwanahararakati wa sasa kaunti ya Bungoma John Wanyama anataka serikali ya kaunti ya Bungoma kufufua kiwanda cha maziwa cha kimalewa.

Akizungumza akiwa wadi ya Mukuyuni eneo binge la kabuchai kwenye hafla  moja ya mazishi Wanyama amelaumu viongozi waliochaguliwa kwa kuwasahau  wananchi na kuacha viwanda muhimu kaunti ya Bungo  kuanguka kikiwemo cha maziwa cha Kimalewa.

"Hii Bungoma  viwanda vyote vimeanguka, hiki cha maziwa pia hakuna kiongozi anakishughulikia, naomba gavana Lusaka na na spika Moses wetangula  wasaidie watu wetu," Wanyama alisema.

Ameelezea kusikitishwa kwake na pia kiwanda cha maziwa cha webuye ambacho hakijaanza kufanya kazi licha ya serikali kutumia pesa nyingi  kukijenga

Wanyama ambaye ametangaza nia ya kuwania useneta mwaka wa 2027 anataka wakaazi wa kaunti ya Bungoma kumchagua viongozi watakaotetea maslahi yao.


Monday, 10 June 2024

PALANG'A AONYA WABUNGE DHIDI YA MSWAADA WA FEDHA

Huku waziri wa fedha Njuguna Ndung’u  akitarajiwa kusoma makadirio ya bajeti ya mwaka 2024/2025,Mwakilishi wadi ya Olkaria Peter Palang’a anataka wabunge kuondoa ushuru kwa bidhaa muhimu.



Akizungumza akiwa Bokoli kaunti ya Bungoma  Palan’ga amesema  serikal inawadhulumu wananchi kwa kuongeza ushuru wa bidhaa muhimu licha ya Rais Willia Ruto kuahidi kwamba angewasaidia kupunguza ghrama ya maisha

“Kuna watu wanamdanganya Rais na kumshauri apandishe ushuru wa bidhaa muhimu, tunamuomba akumbuke ahadi alizotoa kwa mwananchi wa kawaida wakati wa kampeni,” Palang’a alisema.

Palang’a ambaye amekuwa mwakilishi wadi wa Olkaria kwa miaka 20 anataka wabunge kuangazia mswada wa fedha wa Mwaka wa 2024/2025  akisema watakuwa na maswali ya kuwajibu wakenya waliowachagua.

“Wabunge wetu tunawasihi muangazie kilio cha wakenya, wanaumia na gharama ya ju ya maisha na kuongeza ushuru mwingine kutaendelea kuwaumiza zaidi,” aliongeza

Palanga alisema haya kwenye hafla ya kufuzu kwa wanafunzi wa masomo ya teknolojia kutoka eneobunge la Webuye Magharibi.

Kwenye mradi huo zaidi ya wanafunzi mia tano wamepokea mafunzo ya  teknolojia yanayofadhiliwa na Peter Palang’a huku akitaka vijana zaidi kujitokeza ili wanufaike na masomo hayo .



BUNGOMA HAINA SENETA MCHAPAKAZI-WANYAMA ADAI

 Mwanaharakati wa siasa John Wanyama anataka wakaazi wa kaunti ya Bungoma kuchagua viongozi walio na uwezo wa kuwawakilisha vyema Bungeni.



Akizungumza katika hafla moja ya mazishi Malaha Webuye Magharibi Wanyama amewasuta Wabunge na maseneta kwa kushindwa kumtetea mwananchi wa kawaida na badala yake kuwakilisha tumbo zao Bungeni.

"Munaona gharama ya maisha inapanda kwa sababu ya wabunge tuliowachagua, wanaruhusu serikali kupandisha bei ya bidhaa muhimu na kumnyanyasa mwananchi", Wanyama alisema.

Wanyama ambaye pia ametangaza azma yake ya kuwania kiti cha useneta kaunti ya Bungoma anasema seneta wa sawa David Wakoli hana makali ya kumtetea mkaazi wabungoma katika bunge la seneti.

Anataka wakaazi kumchagua kwenye uchaguzi mkuu ujao akisema seneta wa sasa ameshindwa kutekeleza wajibu wake.

Ameongza kiwa kaunti ya Bungoma kwa sasa Haina mwangalizi wa serikali jambo ambalo linaruhusu ufisadi kuendelea

Friday, 10 May 2024

WAT 2 WAAGA BAADA YA KUOKOLEWA KUTOKA JENGO LA KANDUYI


Serikali ya kaunti ungoma imedhibitisha kwamba watu wawili wameaga dunia kufuatia mkasa wa jengo ambalo liliporomoka walipokuwa wakijaribu kuokota vyuma kuuu eneo la kanduyi.

Kwenye ujumbe wake kwa vyombo vya habari gavana wa kaunt ya Bungoma Keneth Lusaka anasema  wiwili hao waliokolewa na maafisa wa mikasa kaunti ya Bungoma na waliaga walipokuwa wakipokea matibabu.

Ripoti kutoka hospitalini inaashiria kwamba wawili hao waliaga baada ya kupoteza damu nyingi.

Gavana Lusaka ameagiza uchunguzi kufanywa na kubaini kwanini jengo hilo halikuangushwa jinsi ilivyokuwa imeratibiwa.

Ameongeza kuwa serikali ya kaunti itawajibikia mazishi ya wawili hao.

 

VUGUVUGU LA MAZINGIRA CONSERVATION LAPANDA MICHE YA MITI 3000 WEBUYE

Kikundi cha kulinda mazingira cha “Mazingira Conservation” kiomeongoza zoezi la upanzi wa miti eneo bunge la Webuye magharibi huku wakipanda zaidi ya miche elfu tatu katika shule eneo hilo.



Mwenyekiti wake Edward Kimakwa anasme kuwa wamekuwa wakiendeleza zoezi la upanzi wa miti katika shule na makanisa eneo hilo na agizo la raisi la kupanda miti linawiana na ajenda ya vuguvugu hilo.

Kimakwa amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Bungoma kupanda miti kwa wingi akiwataka kupunguza ukataji wa miti kiholela.

“Tumekata miti  kwa wingi na huenda kizazi kijacho kikaathirika, kwa sasa hata kuna aina fulani za wanyama na ndege ambao wameadimika kutokana na uharibifu wa mazingira,” Kimakwa alisema

Mwanamazingira huyo ametoa wito kwa viongozi waliochaguliwa kutenga pesa na kununua miche ambayo inaweza kupeanwa kwa wakulima bure ili wapanda.

Ametaka pia serikali ya kitaifa kutobagua waathiriwa wa mvua kaunti ya Bungoma wakati wa kupeana msaada.

“Tuna wakaazi wengi kaunti yetu ya Bungoma walioathirika na mvua inayoendelea, baadhi yao nyumba zimeanguka na wengine mimea yao imeharibiwa na mafuriko, naomba  rais William Ruto  ahakikisha watu wetu pia wanafidiwa kwa hasara waliopata,” Kimakwa alisisitiza.

Kauli yake imeungwa mkono na chifu wa kata ya Miendo Carolye Lwiki  na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya miendo Christine makamu waliowataka wakaazi wa eneo hilo kutumia mvua inayonyesha kwa sasa kupanda miti kwa wingi.

Nao baadhi ya vijana wa kikundi hicho wakiongozwa na katibu wao Nickson Machani wamewataka vijana wenzao kukumbatia upanzi wa miti wakisema huenda ikawanufaisha siku za usoni.

“Vijana wengi hukata tu miti lakini hawakumbuki kupanda, ndio sababu kupitia kwa mfadhili wetu Edward Kimakwa tunapanda miti ili kulinda kizazi kijacho,” Machani alisema


Haya yanajiri wakati ambao taifa la Kenya linashuhudia mvua nyingi huku mamia ya watu wakiathirika  na wengine kuaga dunia.

 

WAHOFIWA KUAGA BAADA YA KUANGUKIWA NA JENGO KANDUYI

Vijana waliokuwa wakiokota vyuma kuukuu kwenye jengo la Wangamati wamefunikwa na vifusi ikihofiwa kwamba huenda wameaga dunia baada ya jengo hilo kuporomoka.

Miongoni mwao ni vijana wanaorandaranda mitaani waliokuwa wakiokota vyuma kutoka eneo hilo.

serikali ya kaunti ya  Bungoma ilianza ubomozi wa jengo hilo linalomilikiwa na familia ya aliyekuwa gavana wa kaunti ya Bungoma Wycliffe Wangamati.

Aliyekuwa gavana Wycliffe wangamati ameisuta serikali ya kaunti kwa utepetevu wake   ambao umepelekea maafa hayo.

kwenye mtandao wake wa kijamii wangamati na Nduguye Winston Wangamati 
wametaka serikali ya kaunti kuwajibikia maafa hayo.


shughuli za uokozi zinaendelea  huku kitengo cha kukabiliana na mikasa kaunti ya Bungoma kikiwa katika njia panda kwa kukosa vifaa vya kukabiliana na mikasa

Thursday, 9 May 2024

AFUENI YA MAJI SAFI MLIMA ELGON

Wakaazi zaidi ya elfu mia moja kutoka mlima elgon, kabuchai na kanduyi  watanufaika na maji safi  baada ya serikali ya kaunti ya Bungoma kwa ushirikiano na  serikai ya Korea kuzindua mradi wa maji eneo la  mlima elgon.



Mradi huo wa maji uliozinduliwa na balozi wa taifa la Korea Yeo Sung-Jun  na gavana wa kaunti ya Bungoma Keneth Lusaka  unalenga kuongeza idadi ya wakaazi wanaopata maji safi ya matumizi.

“Huu mradi wa KOICAII utafaidi wakaazi wetu hapa Mlima Elgon na maeneo bunge jirani kama Kabuchai na kandui na tunalenga kuzindua miradi zaidi ya maji.” Gavana Lusaka alisema.

Balozi wa taifa la Korea amesema mradi huo umegharimu shilingi mlioni mia sita na hivi karibuni  taifa hilo litashirikiana na serikali ya kaunti ya Bungoma kuanzisha mraidi wa KOICA III .



Swala la maji limekuwa donda sugu kwa wakaazi wa kaunti ya bungoma licha ya kuwa na vyanzo vingi vya maji.

Tuesday, 7 May 2024

KITENDAWILI CHA WANGAMATI’S

Familia ya aliyekuwa gavana wa kaunti ya Bungoma Wycliffe wangamati inakadiria hasara baada      ya jumba 

la dhamani ya mamilioni ya pesa kubomolewa kufuatia ujenzi wa uwanja wa Masinde Muliro unaoendelea.

Ujenzi huo unalenga kukamilika kabla ya sherehe za madararka huku serikali ya kaunti ya Bungoma ikibomoa majengo yanayokaribia uwanja wa masinde Muliro.


Familia ya Wangamati Ikiongozwa na aliyekuwa gavana Wyclife Wangamati imekashifu  hatua hiyo ikisema ilipata ardhi hiyo kisheria.

Patrick wangamati ambaye ni mmiliki wa jengoi hilo anasema kuwa alifuata sheria mwaka wa 1968 kupata ardhi hiyo kwa ajili ya Biashara.

“Mimi sio mwizi wa Mashamba, nilifuata sheria na serikali ikanipa ardhi hii na nimekuwa nikiendeleza bisharazangu mahali hapa, nashangaa kwanini wanabomoa nyumba yangu,” Mzee wangamati alisema.

Ubomozi huo umeibua hisia mseto kutoka kwa wafuasi wa aliyekuwa gavana Wycliffe  Wangamati wakimtuhumu gavana Keneth Lusaka na spika Moses Wetangula kwa kumulenga  kisiasa.

Hata hivyo mradi wa ujenzi wa uwanja wa Masinde Muliro ulianzishwa na aliyekuwa gavana Wycliffe Wangamata alipokuwa uongozini. Wakati uo huo alianzisha ujenzi wa barabara kuu mjini Bungoma maarufu kama (dual carriage).

Wangamati alinukuliwa akisema kuwa wale wote waliojenga kwenye ardhi ya serikali waondoe majenge  hayo ili kuruhusu ujenzi wa miradi hiyo miwili mikuu la sivyo serikali itekeleze ubomozi huo.

Wapinzani wake wanadai kuwa alinuia kutumia wadhifa wake kujilinda dhidi ya ubomozi huo.





Thursday, 18 April 2024

Mradi wa kukabili Radi-Nabuyole

 Mbunge wa webuye Mashariki Martin Wanyonyi amezindua mradi wa shilingi milioni tatu kukabiliana na Radi eneo la Nabuyole.

Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo Katika shule ya msingi ya Nabuyole Wanyonyi amesema mitambo ya radi itaepusha maafa yanayotokea wakati wa mvua.

"Tutaweka vivaa vya kisasa kuzuia radi eneo hili, nimeagiza mkandarasi kuhakikisha mradi huu unaisha haraka," Wanyonyi walisema. 

Wakaazi  eneo hilo wamepongeza  hatua hiyo wakisema ni afueni kwao











Sunday, 7 April 2024

𝐋𝐮𝐬𝐚𝐤𝐚 𝐔𝐫𝐠𝐞𝐬 𝐅𝐨𝐫𝐦𝐚𝐭𝐢𝐨𝐧 𝐨𝐟 𝐑𝐨𝐛𝐮𝐬𝐭 𝐌𝐮𝐥𝐞𝐦𝐛𝐞 𝐂𝐚𝐮𝐜𝐮𝐬 𝐟𝐨𝐫 𝐑𝐞𝐠𝐢𝐨𝐧𝐚𝐥 𝐄𝐦𝐩𝐨𝐰𝐞𝐫𝐦𝐞𝐧𝐭.



𝑩𝒚 𝑬𝒍𝒊𝒛𝒂𝒃𝒆𝒕𝒉 𝑲𝒂𝒌𝒂𝒊/𝑮𝑷𝑼


Bungoma Governor Kenneth Lusaka of has called upon the political leadership in the Western region to establish a formidable caucus aimed at fostering socio-economic advancement.


 Speaking at a church service in Kakamega County, Governor Lusaka emphasized the importance of collaboration among leaders for the collective benefit of their constituents.


"In order for our region to prosper, it is imperative that we establish a strong political caucus and foster cooperation, as these are essential instruments in driving forward our developmental aspirations for the people," he remarked.


Lusaka issued a challenge to the Mulembe Nation, urging them to invest in current leadership to bolster the region's prominence on the national stage. 


"We must take pride in our region's top leadership and rally behind our own to bolster our bargaining power for a fair share of the national resources," he concluded. 

𝓟𝓱𝓸𝓽𝓸𝓼 𝓐.𝓢𝓲𝓯𝓾𝓷𝓪 /𝓖𝓟𝓤


Friday, 2 February 2024

MWANAFUNZI ALILIA JOHN MAKALI NA MAKABICHI

 

Mwanafunzi mmoja kwa jina Joseph Owino kutoka Musikoma eneobunge la Kanduyi kaunti ya Bungoma  amejiwasilisha katika shule ya wavulana ya Ndivisi   akiwa na barua yake pekee, bila mzazi, na vifaa muhimu vya masomo.

Joseph Owino 


Owino ambaye ni alipata alama 338  katika shule ya Moi Primary anasema juhudi zake za kupata msaada kutoka kwa eneobunge la CDF la Kanduyi ziligonga mwamba na alipoona siku za kuripoti zinaisha aliamua kutembea kwa miguu kutoka Musikoma hadi Shule ya Wavulana ya  Ndivisi eneobunge la Webuye Mashariki.

mamangu huchoma Mahindi na nina Ndugu zangu ambao pia wanamtegemea, alijaribu kutafuta karo lakini njia zote zikashindikana,” Owino alisema.

Owino ambaye alikuwa tu na barua na sare ya shule ya msingi na patipati zilizochanika  anatoa wito kwa wahisani akiwemo mbunge wa Kanduyi John Makali na gavana wa kaunti ya Bungoma Keneth Lusaka kumsadida ili alipe karo na kumuwezesha kutimiza ndoto yake ya kuwa daktari.

“Mbunge Wangu Joh Makali naomba unihurumie unisaidie hata Basari niendelee na masomo yangu nikuwe Daktar.” Alisema

Aemuomba wakilishi wadi eno hilo Bw Makabichi pia kumsaidia afanikishe donto zake.

Mwalimu mkuu wa shule ya Wavulana ya  Ndivisi Martin Wachiye alimpokea mwanafunzi huyo lakini anatoa wito kwa wahisani kujitokeza na kumlipia karo ili atimize ndoto yake.