Wednesday, 10 June 2020

AOMBA MBUNGE WA KIMILILI DIDMUS BARASAUSAIDIZI WA KULIPIA MATIBABU HOSPITALINI

Huku janga la Covid 19 likiendelea kuswasonga wakenya Masaibu ya Timothy Wanjala Kutoka Kimilili yanazidi kuongezeka baada ya mkewe kulazwa katika hospitali ya Webuye huku   akizuiliwa kwa kwa kushindwa kulipia ada ya shilingi 7,000/=
TIMOTHY WANJALA NA MKEWE CARLYNE
NEKESA HOSPITALINI WEBUYE


Wanjala ambaye ni mkaazi wa Bahai eneo bunge la Kimili anasema wamekuwa wakipitia hali ngumu ili kugharamia matibabu ya mkewe
Timothy Wanjala  Simiyu ambaye pia ana ulemavu wa macho anasema mkewe  Carolyne Nekesa alilazwa na kufanyiwa upasuwaji mkononi ili kuondoa uvimbe lakini  baada ya matibabu hayo hawana njia nyingine ya kulipia matibabu  hayo wakitoa wito kwa wahisani kuingilia kati na kuwasaidia ili warejee nyumbani.
“ Nimejaribu kutumia kadi yangu ya NHIF lakini imeshindikana baada ya usimamizi wa hospitali ya Webuye kuniambia kuwa sijalipia kadi hiyo kwa muda wa miezi kumi na miwili ijayo, sasa sina jinsi nitakavyolipia matibabu ya mke wangu,” Wanjala alisema
Kwa sasa Wanjala na mkewe wamezuliwa katika hospitali ya Webuye akisema  kuzuiliwa kwake kumefanya hana jinsi ya kutafuta pesa hizo ili amlipie mkewe  gharama za matibabu.
“Nimeshindwa jinsi nitakavyomsadia mke wangu, mimi mwenye sina uweza wa kuona hata nikiondoka hapa sijui nitaanzia wapi ndiposa nipate pesa hizo, naomba munisaidie mimi na mke wangu turudi nyumbani tuangalie watoto wetu,” alisema.
Wanjala ambaye ni baba wa watoto saba anasema tangu mkewe aanze kuugua na kusambaa kwa ugonjwa wa Covid 19 nchini  wamekuwa wakipitia hali ngumu kukidhi mahitaji ya wanao 7  pamoja na matibabu ya mkewe.

“Sai wanangu hawana mlezi nyumbani, naomba Mbunge wangu mpoendwa Didimus barasa na Mca wangu au mtu anayeweza kunisadia tu nilipe hizi pesa, nikiondoka nitajua jisni ya kujipanga,” aliomba.
Nambari ya Timothy Wanjala 0711626847

No comments:

Post a Comment