Jamii ya Watachoni imegawanyika kuhusiana na hatua ya Baraza
la wazee wa jamii hiyo kujitokeza na kusema kuwa wanaunga mkono gavana wa kaunti ya kakamega Wycliffe Oparanya na waziri Eugine wamalwa
kuwa waswemaji wa jamii ya waluhya.
Baada ya kikao cha faragani katika shule ya upili ya Lukusi na
waziri Eugene Wamalwa, gavana Wycliffe Oparanya, Wycliffe Wangamati na sospiter
ojamong’ wazee wa TAKUSO wakiongozwa na
Se Wekesa wamesema kuwa watmuunga mkono rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa
ODM Ralia Odinga kwenye mchakato wa BBI
kabla ya uchaguzi wa 2022, huku baadhi ya wazee wakisema kuwa hawakuhusishwa
katika uamuzi huo.
“tumeamua
kwa kauli Moja kuunga mkono hatua ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga
kuunganisha taifa na tunaomba jamii ya
Tachoni, sote tuunge mkono serikali yetu.” SeWekesa alisema.
Hata hivyo mugawanyiko umeshuhudiwa miongoni mwa wazee hao
huku baadhi ya wazee Watachoni wakisema mkutano huo haukuhusisha viongozi wote.
Wazee hao na baadhi ya wakazi wamesema viongozi wa TAKUSO wanajitakia
wenyewe na mkutano huo ulilenga kunufaisha
wachache.
Wakati uo huo mamia ya wakaazi walifurika katika shule ya upili ya Lukusi wakitarajia kupokea chakula kutoka kwa Waziri Eugene wamalwa huku watu Kumi wakipokea gunia la 50kg la maharagwe na mafyta Lita moja ya kupika.
Wazri huyo na magavana
Oparanya, Ojamong’ na gavana Wangamati waliendeleza siasa za BBI kwa kisingizia
cha kugawa chakula huku wakaazi wakifurika katika uwanja wa shule ya upili ya
Lukusi bila kujali Sheria za kuzua maambukizi ya Covid 19.
Wanne hao wametoa wito kwa jamii ya Tachoni kuunga mkono
mrengo wa Handshek wakisema mrengo wa Tangatanga hautaweza kuwapa maendeleo.
“tunataka jamii ya Mlembe iwe serikali, na Mimi na mwenzangu
Oparanya ndio tuko katika nafasi Bora ya kuwatetea serikali,” waziri wamalwa
alisema.
No comments:
Post a Comment