Thursday, 11 June 2020

LONYANGAPUO AONYWA NA KANU

Kamati ya Kitaifa ya Nidhamu ya Chama cha KANU imemwonya Gavana wa Kaunti ya Pokot Magharibi, Profesa John Lonyang'apuo dhidi ya kutatiza juhudi ya kuwaadhibu wakilishi wadi kumi na wawili ambao wamekiuka kanuni na Katiba ya chama.



Mwanachama wa kamati hiyo, John Ngunjiri amesema kwa sasa kamati hiyo haijapokea agizo la kumwagiza Lonyang'apuo kufika mbele ya kamati hiyo na kusisitiza kwamba kila mwanachama sharti azingatie kanuni za chama.

Wakati wa kikao na wanahabari mjini Kitale katika Kaunti ya Trans Nzoia, Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Zipporah Kitony amesema  wakilisha hao kumi na wawili wa Kaunti ya Pokot Magharibi waliagizwa kufika mbele ya kamati hiyo na kuhojiwa kwa kutaka kumbandua mamlakani kiongozi wa wengi wa bunge, Thomas Longolesia hilo kinyume na msimamo wa chama

No comments:

Post a Comment