Sunday, 14 June 2020

MUSIINGIZE SIASA KATIKA KUTEULIWA KWA PROF SIAMBA-WETANGULA AMWAMBIA ESELI


Seneta wa kaunti ya Bungoma Moses Wetangula amepuuzilia mbali madai ya Mbunge wa Tongaren Eseli Simiyu  kuwa mrengo wake ulichangia kuteuliwa kwa naibu Chanzela wa Chuo kikuu cha Kibabi Prof. Dolnald Siamba.


Wetangula anasema waziri Eugine Wamalwa, Eseli Simiyu na Mbunge wa Kanduyi Wafula Wamunyinyi hawakuhusika kwa vyovyote katika kuteuliwa kwa Siamba akisema wanajaribu kutumia swala hilo kujinufaisha kisiasa.
“ Kama Wamalwa yuko Serikalini alikuwa anaenda kumuona Raila kama nani? Raila odinga hayuko serikalini na hana uwezo wowote wa kumteua mtu katika wadhifa wa taasisi za uma,” Wetangula alisema.
Wetangula amesema kuwa ni yeye aliyefanya mazungumzo na maafisa wakuu serikalini kuhakikisha kuwa Siamba anateuliwa.
Wetangula pia amesema chama cha Ford Kenya kitawachukulia hatua za kinidhamu Eseli, Wamunyinyi na Wangamati kwa kujaribu kufanya mapinduzi chamani.
Hata hivyo mrengo wa Eseli umeshikilia kuwa haumtambui Wetangula kama kinara wa chama cha Simba.

No comments:

Post a Comment