Friday, 12 June 2020

SENETI HAITAMBANDUA GAVANA ANNE WAIGURU

Mchanganuzi wa maswala ya kisiasa John Wanyama amesema itakuwa vigumu kwa bunge la seneti kumbandua gavana wa Kirinyaga Anne waiguru kutokana na ushawishi wake serikalini.

Wanyama amesema kutokana na uhusiano ambao Gavana  huyo  anao na rais Uhuru Kenyatta pamoja na  kinara wa ODM Raila odinga huenda maseneata wakamnusuru  baada ya wawakilishi wadi wa kirinyaga kupitisha mswaada wa kumuondoa afisini.

“Tumeona Bi Waiguru akidhihirisha uwezo wake wa kuwa msemaji wa jamii ya Kikukuyu na uhusiano wake wa karibu na RailaOdinga  huenda ukapelekea maseneta wanaoegemea mrengo wa ODM na rais Uhuru Kenyatta kupinga kubanduliwa kwake jambo,ambalo litamrejesha afisini.” Wanyama alisema.

Wanyama ameongeza kuwa ikiwa Bunge la seneti litamrejesha afisini huenda akawa na usemi katika uchagusi wa urais mwaka wa 2022, na kuvutia wawaniaji wa urais kuunda muungano naye.

 

JOHN WANYAMA

No comments:

Post a Comment